Romans 3:9-14

9 aTusemeje basi? Je, sisi ni bora kuwaliko wao? La hasha! Kwa maana tumekwisha kuhakikisha kwa vyovyote kwamba Wayahudi na watu wa Mataifa wote wako chini ya nguvu ya dhambi. 10 bKama ilivyoandikwa: “Hakuna mwenye haki, hakuna hata mmoja.

11 Hakuna hata mmoja mwenye ufahamu,
hakuna hata mmoja amtafutaye Mungu.

12 cWote wamepotoka,
wote wameoza pamoja;
hakuna atendaye mema,
naam, hakuna hata mmoja.”

13 d“Makoo yao ni makaburi wazi;
kwa ndimi zao wao hufanya udanganyifu.”
“Sumu ya nyoka iko midomoni mwao.”
14 e“Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.”
Copyright information for SwhKC